Christian movie “Siri ya Utauwa: Mfuatano” | Preaching the Gospel of the Second Coming of Lord Jesus
Christian movie “Siri ya Utauwa: Mfuatano” | Preaching the Gospel of the Second Coming of Lord Jesus
10 Nov
Christian movie “Siri ya Utauwa: Mfuatano” | Preaching the Gospel of the Second Coming of Lord Jesus
Lin Bo'en ni mhubiri mzee ambaye amemwani Bwana kwa miongo mingi. Tangu alipomkubali Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, alihukumiwa, akatengwa, na akafukuzwa kutoka kwa jumuiya ya kidini na wachungaji na wazee wa kanisa, nguvu zinazompinga Kristo. Lakini ingawa Lin Bo’en alishambuliwa, akahukumiwa na kusingiziwa, hakusita kwa woga. Badala yake, imani yake ikawa thabiti zaidi kuliko ilivyowahi kuwa, na hili lilimwongoza kufahamu hatimaye kwamba wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini walikuwa wakiigiza kwa udanganyifu sura adilifu. Wakati huo huo, alikuja kujua kwamba Kristo pekee ndiye ukweli, njia, na uzima, na Kristo pekee ndiye Anaweza kumwokoa na kumtakasa na kumkamilisha mwanadamu. Kwa ajili ya hili, aliamua kumfuata Kristo, kumshuhudia Kristo, na kufanya kila linalowezekana kufuatilia ukweli, kutafuta kuigeuza tabia yake ili aweze kuwa shahidi wa kweli wa Mungu. Mara tu Chama cha Kikomunisti cha Uchina kilipogundua kwamba Lin Bo’en aliachiliwa kutoka gerezani na hakuwa amebadilika, kwamba hakuwa ameikana imani yake hata kidogo na hata aliamini katika Umeme wa Mashariki, kwamba alienda kila mahali kushuhudia kwamba Bwana Yesu amerudi tena na kwamba Yeye ni Mwenyezi Mungu, CCP kilimworodhesha kama mtu wa kutakiwa na walienda kila mahali kumkamata. Lin Bo’en alilazimika kuiacha familia yake, na kila mahali aliposhuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, aliweza kuwaongoza waumini wengi waaminifu, wa tabia njema kwa upande wa Mungu. Video hii inatoa maelezo ya hadithi ya kweli ya Lin Bo’en ya kueneza injili na kumshuhudia Mungu.
Zaidi: Sehemu Siri za kuja kwake Yesu Kristo kwa mara ya pili inalenga kujadili nawe ukweli na siri kuhusu kuja kwake Yesu Kristo kwa mara ya pili, ikiwa ni pamoja na njia ambayo Bwana Yesu Atakuja tena nayo na kile Bwana Yesu Atafanya atakapokuja tena, na kadhalika, ambayo ni muhimu kwetu kukaribisha kuja kwake Yesu kwa mara ya pili.