Umati unanishangilia, umati unanisifu; watu wote wanalitaja jina la Mungu mmoja wa kweli, watu wote wanayainua macho yao kuviangalia vitendo Vyangu. Ufalme unashuka duniani mwa wanadamu, nafsi Yangu ni ya fahari na yenye neema. Nani asingesherehekea kwa ajili ya hili? Ni nani asingecheza kwa furaha? Ee Sayuni! Inua bendera yako ya ushindi unisherehekee! Imba wimbo wako wa ushindi ili ulieneze jina Langu takatifu! Viumbe wote duniani kote! Harakisheni kujitakasa ili muweze kufanywa kuwa sadaka Kwangu! Nyota juu mbinguni! Rudini kwenye maeneo yenu kwa haraka ili muonyeshe nguvu Yangu kuu katika anga! Nazisikiliza sauti za watu duniani, wanaomimina upendo na uchaji wao mwingi kwa ajili Yangu katika wimbo! Katika siku hii, huku viumbe wote wakirudishiwa uhai, Nashuka katika dunia ya wanadamu. Katika wakati huu, mambo yalivyo, maua yanachanua kwa wingi, ndege wote wanaimba kwa sauti moja, vitu vyote vinajawa na furaha! Kwa sauti ya saluti ya ufalme, ufalme wa Shetani unaanguka, ukiangamizwa katika mngurumo wa wimbo wa ufalme, usiinuke tena!
Nani duniani anathubutu kuinuka na kupinga? Ninaposhuka duniani Naleta kuchoma, Naleta ghadhabu, Naleta maafa ya aina yote. Falme za dunia sasa ni ufalme Wangu! Juu angani, mawingu yanagaagaa na kujongea kama mawimbi; chini ya anga, maziwa na mito yanatapakaa na kutoa muziki wa kusonga kwa furaha. Wanyama wanaopumzika wanaibuka kutoka kwenye matundu yao, na watu wote ambao wamelala wanaamshwa nami. Siku ambayo watu wote wameingojea hatimaye imefika! Wananiimbia nyimbo nzuri sana!
Katika wakati huu mzuri, katika wakati huu wa kusisimua,
sifa zinatoka kila mahali, juu mbinguni na chini duniani.
Nani asingesisimka kwa ajili ya hili?
Ni moyo wa nani usingechamka?
Ni nani asingelia kwa sababu ya tukio hili?
Anga si anga ilivyokuwa hapo awali, sasa ni anga ya ufalme.
Dunia si dunia ilivyokuwa hapo awali, sasa ni dunia takatifu.
Baada ya mvua kubwa kupita,
ulimwengu mchafu wa kale unafanywa upya kabisa.
Milima inabadilika … maji yanabadilika …
watu pia wanabadilika … vitu vyote vinabadilika….
Aa, milima iliyo mitulivu! Inukeni na mnichezee!
Aa, maji yaliyotuama! Endeleni kutiririka kwa wingi!
Ninyi wanadamu mnaoota ndoto! Jiinueni na mkafuate!
Nimekuja … Mimi ni mfalme….
Wanadamu wote watauona uso Wangu kwa macho yao wenyewe,
wataisikia sauti Yangu kwa masikio yao wenyewe,
watafurahia wenyewe maisha katika ufalme….
Matamu sana… mazuri sana….
Yasiyosahaulika … yasiyoweza kusahaulika….
Katika mwako wa hasira Yangu, joka kubwa jekundu linapambana;
katika hukumu Yangu adhimu, pepo wanaonyesha sura zao za kweli;
kwa maneno Yangu makali, watu wote wanaona aibu sana,
na hawana popote pa kujificha.
Wanakumbuka zamani, jinsi walivyonidhihaki na kunikejeli,
Hakukuwahi kuwa na wakati ambapo hawakujiringa,
hakukuwahi kuwa na wakati ambapo hawakuniasi.
Leo, nani halii? Nani hahisi majuto?
Ulimwengu dunia wote umejawa machozi …
umejawa sauti za kushangilia … umejawa sauti za vicheko….
Tazama zaidi:Mkusanyiko wa sinema zetu bora za injili. Hizi shuhuda za kweli ulionenwa na kazi Yake ya hukumu ya Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho zitakuongoza kuelewa kazi ya Mungu ya siku ya mwisho na kukaribisha kurudi kwa Bwana.