Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu
Mwenyezi Mungu anasema:
Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu. Kuhusiana na kumjua Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, sehemu ya kwanza tuliyoijadili ni ipi? (Mamlaka ya Mungu.) Ya pili ilikuwa ni ipi? (Tabia ya haki ya Mungu.) Na ya tatu? (Utakatifu wa Mungu.) Tumejadili mara ngapi kuhusu mamlaka ya Mungu? Je, imewacha wazo kwako? (Mara mbili.) Je kuhusu tabia ya haki ya Mungu? (Mara moja.) Idadi ya safari tulizojadili utakatifu wa Mungu pengine imeacha wazo kwako, lakini maudhui mahususi tuliyojadili kila mara yamewacha wazo kwako?
Makala Yaliyopendekezwa: Neno la Mungu “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu”